Uchaguzi wa wakati na mazingira wakati wa uleaji wa malkia.

October 21, 2026 Apiologist sanga.

Uchaguzi wa wakati na mazingira kipindi cha uleaji wa malkia.

 

Kwanza kabisa ni vema kujua maana ya jumla ya neno Queen rearing,

 

Kwa tafsiri isiyo rasmi ya kiswahili, Queen rearing ni Uleaji wa malkia wa nyuki  huu ni mchakato wa kukuza malkia wapya wa nyuki kutoka kwenye mayai yaliyorutubishwa (lava wachanga watakaokuja kuwa nyuki jike wanaoweza kuwa malkia) ili kuchukua nafasi ya malkia wazee, malkia wasioweza kufanya majukumu yao ya kawaida, kuongeza ukubwa wa kundi ndani ya mizinga, au kuboresha tija kama vile uzalishaji mkubwa wa asali na utulivu wa nyuki. (hizi ni sababu muhimu pia za kwanini tunafanya uleaji wa malkia)

Blog image



 

 unahitaji usimamizi wa makini wa muda  yaani ratiba ya kila shughuli , kuzingatia hali ya hewa, na rasilimali thabiti za mzinga ili kufanikiwa mchakato huu wa kulea malkia.

Ufuatao ni muongozo wa jumla wa mambo ya kuzungatia wakati wa kufanikisha zoezi la uleaji wa malkia.

 na muongozo huu unaweza kutofautiana kulingana na mbinu utakayoitumia ..

 

1.     Wakati (timing) na hali ya hewa inayofaa.

·      Msimu Bora: Fanya ufugaji wa malkia wakati wa msimu wa maua mengi (wakati kuna nekta na chavua kwa wingi) au weka chakula cha nyongeza (maji ya sukari na mbadala wa chavua). Kwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki, hii kawaida hufanyika wakati au mara baada ya majira ya mvua (kama vile Juni hadi Oktoba/Novemba kutegemea na ukanda wako).

·      Kuwepo kwa Nyuki Madume (Drones): Hakikisha kuna nyuki madume waliokomaa wanaoruka kwenye eneo lako angalau siku 10 hadi 14 kabla ya malkia mpya kutoka kwenye seli zao. Madume huchukua siku 10 hadi 12 baada ya kutotolewa  ili kukomaa kijinsia.

·      Hali ya Hewa ya Kupandana: Malkia anahitaji hali ya hewa ya joto, jua, na kusiwe na upepo mkali (zaidi ya nyuzi joto 20°C) ili aweze kuruka nje na kupandana na madume.

Blog image

2.     Hali ya Mzinga Maalum (Mzinga wa Kuanzia - Starter).

·      Kutokuwepo kwa Malkia: Mzinga unaotumika kuanzisha seli za malkia lazima uwe hauna malkia kabisa na usiwe na mayai au lava wachanga wa nyuki wafanyakazi. Hii inawafanya nyuki wafanyakazi kuelekeza nguvu zao zote kulisha vikombe vya malkia ulivyoweka.

·      Wingi wa Nyuki Walezi (Nurse Bees): Mzinga lazima uwe na nyuki vijana wengi (wenye umri wa siku 5–15) ambao ndio wanaozalisha "Royal Jelly" (chakula cha malkia) kwa wingi.

·      Lishe Bora: Mzinga lazima uwe na akiba kubwa ya chavua (pollen) kwa ajili ya protini na asali au maji ya sukari kwa ajili ya wanga ili malkia wakue vizuri na kuwa wakubwa.

·      Umri wa Lava (Grafting): Kama unahamisha lava (grafting), chagua lava wachanga sana wenye umri wa chini ya saa 72 (bora zaidi wakiwa na saa 12 hadi 24, wale wanaofanana na herufi "C" ndogo sana). Lava wakiwa wakubwa, wanakuwa malkia dhaifu.

Blog image 3.     Ratiba ya Siku 16 ya Ukuaji wa Malkia. ingawa ratiba hii inaweza kuwa na utofauti kulinganisha na aina moja na nyingine nyuki, mazingira yanazunguka na sababu za kijenetikia za nyuki pia. ufuatao ni mfano muongozo wa ratiba inayoweza kuzingatiwa wakati wa mchakato mzima wa kulea malkia. 

·      Siku ya 0: Yai linatagwa.

·      Siku ya 3: Yai linatumbuliwa na kuwa lava mchanga (muda sahihi wa kuhamisha/grafting yai).

·      Siku ya 4 (Siku ya 1 baada ya kuhamisha): Lava wanawekwa kwenye mzinga maalum usio na malkia.

·      Siku ya 9: Seli za malkia zinafungwa (capped) na nyuki walezi.

·      Siku ya 10–12: Seli zilizofungwa zinahamishwa kwa makini kwenda kwenye mizinga midogo (Nucleus/Nucs) ambako watatokea.

·      Siku ya 16: Malkia bikira anazaliwa (anatoka kwenye seli)

·      Siku ya 21–22: Malkia anakomaa kijinsia na kuanza safari za majaribio na kupandana hewani.

·      Siku ya 23–26: Malkia anaanza kutaga mayai. kwa mzunguko uleule ulioelezwa hapo juu...

 

Blog image

Comments

No comments yet. Be the first to comment!

Leave a Comment

My Cart

Your cart is empty

 

 

Resolving Details