Jinsi gani tunaweza kuzuia robbing katika mashamba ya nyuki?..

October 15, 2026 Apiologist sanga.

Kwanza kabisa, inabidi tufahamu maana ya neno robbing.

 

"Robbing" (Kuvamiwa au Kuibiwa asali) katika ufugaji wa nyuki ni tabia ya fujo ambapo nyuki kutoka mzinga wenye nguvu au wenye njaa wanashambulia mzinga mwingine ulio dhaifu ili kuiba asali au rasilimali yoyote iliyo muhimu.

hivyo, kuzuia kitendo hiki katika mzinga au mizinga ndani ya shamba la nyuki, ndivyo tunavyoweza kuzuia katika mashamba ya nyuki. 


Nini Kinasababisha "Robbing" katika mashamba ya nyuki?

  • Uhaba wa Maua (Drought/Dearth period): Hali hii hutokea sana wakati ambapo hakuna maua ya kutosha kwenye mazingira asili, hivyo nyuki wanatafuta chakula mahali popote kinapoweza kupatikana.
  • Mizinga Dhaifu: Mizinga yenye idadi ndogo ya nyuki au malkia mgonjwa (asiyefanya kazi kwa ukamilifu)  inakuwa haina uwezo wa kujilinda dhidi ya wavamizi.
  • Makosa ya Mfugaji nyuki: Kuacha asali au maji ya sukari wazi karibu na mizinga, au kuacha mzinga wazi kwa muda mrefu wakati wa ukaguzi au shughuli nyingine yoyote inayohusu ufunguaji wa mzinga.

 

Dalili za Mzinga Unaoibiwa rasilimali zake kama asali..

  • Vurugu katika Lango la Mzinga: Nyuki wanaruka kwa fujo na kuchanganyikiwa mlangoni.
  • Mapigano: Utaona nyuki wakikandana na kung'atana pembezoni mwa mzinga unaoibiwa au kwenye ubao wa kutua katika mzinga.
  • Nyuki Wafu: Idadi kubwa ya nyuki waliokufa chini karibu na mzinga unaoibiwa.
  • Mlio wa Juu: Mzinga unakuwa na mlio mkali na wa juu wa kilio au fujo za nyuki -high buzzying sounds-.

 

insi ya Kuzuia na Komesha robbing katika mizinga.

  • Kupunguza Mlango: Punguza ukubwa wa mlango wa mzinga ili nyuki walinzi wachache waweze kuulinda kwa urahisi.
  • Kuweka "Robbing Screens": Hizi ni nyavu maalum zinazowachanganya wezi lakini zinaruhusu nyuki wa mzinga husika kuingia.
  • Kulisha kwa Umakini: Lisha nyuki kwa kuweka chakula ndani ya mzinga na sio nje, na usafishe sukari yote inayomwagika.
  • Kupanda miti ya muda mfupi,wa kati na mrefu itoayo maua kwa vipindi tofauti-tofauti.  Hii huweza kufanyika pia wakati wa uchaguzi wa eneo lifaalo kwaajili ya ufugaji nyuki kwa kuangalia aina ya mimea inayoweza kutoa maua kwa vipindi tofauti ili kupunguza ukali wa dearth period.
  • Kufanya kundi la nyuki liwe lenye nguvu. - zipo njia kadhaa za haraka na za kitaalamu ambazo mfugaji wa nyuki  anaweza kuzitumia kuliongezea nguvu na kuokoa kundi dhaifu la nyuki Kama vile Kuhamisha Sega la Mayai/Mabuu (Brood Boosting) ili kuliongezea idadi ya nyuki vibarua kundi lililo dhaifu, Kulisha kundi la Nyuki dhaifu kwa Kutumia Sukari na Poleni (Supplemental Feeding) ili kuchochea malkia kutaga mayai mengi zaidi na kupata chakula cha kuanzia kwa mabuu ya nyuki, Kupunguza Ukubwa wa Mzinga (Downsizing of the hives)

Mzinga mkubwa sana wenye nyuki wachache huwafanya washindwe kudhibiti joto na ulinzi, Kubadilisha Malkia Dhaifu (Requeening) katika kundi dhaifu la nyuki, na mwisho kabisa ni Kuunganisha Mizinga Miwili Dhaifu (Combining Colonies) na kumuacha malkia mmoja alie na nguvu.

 

Blog imageBlog imageBlog image

Comments

No comments yet. Be the first to comment!

Leave a Comment

My Cart

Your cart is empty

 

 

Resolving Details